Tuesday, November 29, 2011

JE, WAJUA.?

Bila shaka ungekuwa na wasiwasi kujibu swali hilo..labda ukifikiri kwamba ni swali gumu sana. Labda ungefikiri, "Je, kweli najua.?" au "Mimi sijui mambo mengi".

Lakini ukweli ni kwamba wewe unajua mambo mengi sana ambayo watu wengine hawafahamu..au kama wapo wanaofahamu, basi ni wachache sana. Hivyo tunapaswa kujiamini ili tunapoulizwa Je, wajua.? tuseme ndio, NINAJUA..
Leo ningependa kuzungumzia jambo moja ambalo huenda hukujua, lakini sasa umejua..

Watu wengi huogopa kutumia simu za mkononi (cellphones) wakati wa radi kwa sababu ya hofu ya kwamba watapigwa na radi. Lakini ukweli ni kwamba simu za waya (cabled phones) ndizo zinazoweza kukupelekea kupigwa na radi kwani umeme wa radi unaweza kupita kwenye nyaya ya simu na kuleta madhara kwa mtumiaji. Lakini simu za mkononi zisizo na nyaya (wireless) ni SALAMA kabisa na hazina uhusiano na radi.!!

Hilo ni jambo moja ambalo umejua, umeliongeza kwenye mengi ambayo tayari unajua. Je, ungependa kujua zaidi.? Bila shaka ungependa.. Basi karibu tena wakati mwingine ambapo tutazidi kuhabarishana na kuchunguza mambo mengine mengi..

**Kwa swali, maoni au maelezo tafadhali tumia anuani ya barua pepe: dakinnie@gmail.com au dakinnie@ovi.com. Pia nina patikana facebook, http://facebook.com/boyvinnie

..enjoy..

No comments:

Post a Comment