Tuesday, November 29, 2011

MAJI YANAUA.!!

"Maji ni uhai.!" Hiyo ni kauli-mbiu ambayo wengi wetu tunaifahamu au sio.? Lakini ushawahi kuwaza kwamba maji yanaweza kuwa kifo.? NDIO!

Maji yanapotumiwa kwa kiasi kinachofaa, yana manufaa makubwa katika miili yetu. Lakini kunywa maji MENGI SANA kwa MUDA MFUPI kunaweza kuua kwani kunapunguza sana kiasi cha madini mwilini kwa muda mfupi na miili yetu haiwezi kustahimili badiliko hilo la ghafla.

Hivyo "kunywa kistaarabu", na sizungumzii pombe...ni maji hayahaya...rafiki wa afya na mazingira lakini ambaye anaweza kuwa muuaji hatari sana..!

4 comments: